[recent]

Chui aingia kwenye gari la Watalii Serengeti, na kufanya haya


Embu pata picha kama upo na familia yako au rafiki zako mmeenda kutembelea kwenye mbuga za wanyama halafu chui anaingia ndani ya gari lenu…! hivyo ndivyo ilivyotokea kwa  Britton Hayes na mjomba wake kutoka  Seattle, Washington, walikuwa safarini kujionea wanyama katika mbuga ya taifa ya Serengeti nchini na chui akaingia kwenye gari lao, chui akawa mtalii ndani ya gari lao.
Mgeni huyo wasiyemtarajia alikaa ndani ya gari hilo kwa dakika 10 katika eneo la Gol Kopjes la mbuga hiyo, kabla ya mwishowe kuondoka kwenda kuwinda swala.
Britton Hayes anasema walikuwa wamemuangazia chui mmoja aliyekuwa ameruka sehemu ya mbele ya gari lao pale mwingine aliporuka na kuingia kupitia sehemu ya nyuma bila wao kumuona.

No comments:

Powered by Blogger.