[recent]

Wizkid aanza rasmi safari ya matumaini

Wizkid aanza rasmi safari ya matumaini

Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid ameanza safari yake rasmi ya kushoot video zake zote ndani ya bara la Afrika kama alivyotangaza wiki iliyopita.
Wizkid
Wizkid alinukuliwa kwenye kituo cha Beat 99.9 FM cha jijini Lagos, Nigeria akisema kuwa kuanzia mwaka huu hata-shoot tena video nje ya nchi na kutangaza kuwa video zote ambazo ameshamaliza kushoot nje ya bara la Afrika ameshazipiga chini.
Jana Davido ameudhihirishia umma juu ya kauli yake hiyo kwa kuachia video yake ya kwanza kwa mwaka huu ‘SOCO’ ambapo kichupa hicho kimeongozwa na Clarence Peters na video yote imechukuliwa na jijini Lagos.
Hatua ya Wizkid kutangaza tamko la kusitisha kushoot videozake  nje ya bara la Afrika, imeungwa mkono na Wanaijeria kwani wanaamini kuwa huu ni muda wa kuitangaza zaidi Afrika kwani kuna maeneo mengi na mazuri ya kushoot.

No comments:

Powered by Blogger.