Mchungaji akamatwa na Polisi akijaribu kumfufua Marehemu
Stori ninayokusogezea leo March 28, 2018
ni kumhusu Mchungaji mmoja ambaye amejikuta akiingia mikononi mwa
Polisi baada ya kushindwa kumfufua mwanaume mmoja eneo la kati huko
Msumbiji.
Mchungaji huyo alidai kuwa roho
mtakatifu alimwambia asafiri hadi katika hospitali inayofahamika kwa
jina Chimoio iliyopo katika jimbo la Manica, ili akafanye muujiza ambao
alidai ana uwezo wa kufanya na alipowashawishi Maafisa wa hospitali
walimruhusu aingie ndani ya chumba cha kuhifadhi maiti ili atekeleze
muujiza huo.Hata hivyo baada ya siku mbili za maombi, hakuweza kurejesha uhai wa marehemu na familia hiyo haikushangazwa na kushindwa kwake.
Dada wa marehemu ambaye hakutaka jina lake litajwe aliwaambia waandishi wa habari kuwa “Kasisi aliomba, akaomba na kuomba hadi akanena kwa lugha. Alizungusha kichwa cha marehemu huku na kule huku akiomba.
“Lakini hakuna hata sehemu ya marehemu kaka yangu iliyoweza kutikisika. Wakati mmoja kasisi alipaza sauti akisema, ‘amka, kijana wa Mungu!, Hatukuamini angefanya mwujiza wowote. Hii ni kwa sababu hakuwahi, hata wakati mmoja, kuthibitisha uwezo wake wa kumrejeshea mfu uhai wake.” -Dada wa Marehemu
“Tangu wakati huo kasisi alikamatwa na yuko mikononi mwa polisi akishtakiwa kwa kosa la kumkosea heshima mfu. -Dada wa Marehemu

No comments: